Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya uchumi wa dunia bado imeghubikwa na kiza:UM

Hali ya uchumi wa dunia bado imeghubikwa na kiza:UM

Uchumi wa kimataifa uko katika hali mbaya na unapoelekea utakuwa pabaya zaidi wakati mataifa yanayoendelea pia yakishuhudia mdororo amesema afisa wa Umoja wa Mataifa, Jomo Kwame Sundaram, ambaye ni naibu mkuu wa idara ya uchumi na masuala ya jamii ya Umoja wa Mataifa wakati wa uzinduzi wa ripoti ya hali ya uchumi wa dunia na matarajio siku ya Alhamisi.

Amesema hakuna sababu ya kuchipuka pakubwa uchumi katika nchi zilizoendelea kutokana na upungufu wa kile alichokiita hatua imara ya pamoja kushughulikia matatizo ya sasa ya kimataifa ya uchumi hasa barani Ulaya.

Bwana Sundaram ameongeza kuwa hali huenda ikazorota katika nchi zinazoendelea ambazo uchumi wake umekuwa ukitegemea kusafirisha bidhaa kwenda katika mataifa yaliyoendelea.