Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIDO yamtangaza balozi wake kwenda angani

UNIDO yamtangaza balozi wake kwenda angani

Shirika la viwanda na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNIDO limesema kuwa limemchagua mwanaanga Marcos Pontes raia wa Brazil kwenda angani kama balozi wake wa hisani. Katika tangazo lake leo, UNIDO imesema kuwa kuchaguliwa kwa mwanaanga huyo kimezingatia historia yake ya hapo nyuma.

Inaelezwa kuwa wakati wa ujana wake, alikulia katika maisha ya shida na dhiki katika mitaa ya São Paulo, lakini baadaye alifaulu kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanaanga. Shirika hilo linasema kuwa hatua hiyo ni mfano tosha unaotoa shime kwa watu wengine waliopitia mazingira kama hayo.