Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA kujenga shule kwenye ukanda wa Gaza

UNRWA kujenga shule kwenye ukanda wa Gaza

Shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakiimbizi wa kipalestina UNRWA linasema kuwa limebuni ushirikiano na msanifu maarufu wa majengo ambaye atajenga mashule 20 yasiyoathiriwa na mazingira kwenye ukanda wa Gaza.

UNRWA inasema kuwa mashule hayo yatakayogharimu dola milioni mbili kujengwa yatatoa huduma za masomo kwa wanafunzi 800 na mazingira yatakayowaweza wanafunzi kupata elimu bora. Lengo kuu ni kuhakikisha viwango vya juu vya elimu kwenye shule hizo na hamasisho pamoja na heshima kwa mazingira ya nje.