Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwe na ushirikiano kati ya wanajeshi na mashirika ya kibinadamu

Kuwe na ushirikiano kati ya wanajeshi na mashirika ya kibinadamu

Mkuu wa huduma za misaada kwenye Umoja wa Mataifa ameyataka mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu na vikosi vya jeshi kuweka mikakati ya kuporesjha ushirikiano wao wakati wanapotoa huduma kunapotokea majanga ya kiasili.

Katibu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos anasema kuwa ni mambo mengi yanaweza kufanywa na jeshi kwa haraka na kwenye mazingira magumu. Lakini pia amesema kuwa kuwepo kwa wanajeshi kunaweza kufanya kazi ya mashirika ya kutoa hudumu kuwa ngumu. Amos amesisitiza umuhimu wa masharika ya kibinadamu na wanajeshi kuelewana kuhusu majukumu yao na sheria zinazohitajika.