Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mcheza filamu maarufu nchini India ateuliwa balozi mwema wa UNICEF

Mcheza filamu maarufu nchini India ateuliwa balozi mwema wa UNICEF

Mmoja wa wacheza sinema maarufu nchini India hii leo ameteuliwa kuwa balozi mwema wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ili kushirikiana nalo kuwahakikishia watoto lishe bora. Bwana Aamir Khan mwenye umri wa miaka 46 atatumia umaarufu wake katika kuangazia masuala ya lishe nchini India taifa ambalo mmoja kati ya watoto wanakumbwa na utapiamlo.

Balozi huyo ambaye amekuwa akifanya kazi na UNICEF , serikali na watu maarufu kwenye kampeni ya kitaifa amesema kuwa ataangazia watoto walioathirika zaidi nchini India.