Mahitaji ya waathirika wa usafirishaji haramu yazingatiwe:UM

1 Disemba 2011

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu usafirishaji haramu wa watu hususani wanawake na watoto Joy Ngozi Ezeilo ameitaka serikali ya Australia kutoa msukumo katika haki za binadamu na mahitaji ya waathirika wa usafirishaji haramu hasa watoto huku akilipongeza taifa hilo kwa juhudi zake za kupambana na usafirishaji haramu kitaifa na kikanda.

Amesema ingawa taifa hilo limeonyesha kujizatiti kwake kupambana na uhalifu huo lakini bado haina mipango ya kitaifa ya kukomesha usafirishaji haramu wa watu. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter