Mabadiliko ya hali ya hewa yana athari kwa wahamiaji:UNESCO

1 Disemba 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limesema mabadiliko ya hali ya hewa yana athari kubwa kwa wahamiaji duniani. Pilar Alvarez-Laso naibu mkurugenzi mkuu wa masuala ya jamii na sayansi ya binadamu katika shirika hilo ameyasema hayo katika taarifa ya wahamiaji na mbadiliko ya hali ya hewa iliyoidhinishwa na mashirika 15 ya Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwenye mkutano unaoendelea mjini Durban Afrika ya Kusini .

Taarifa hiyo inasema mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri kundi hili la watu wakiwemo wanawake, watu kutoka makabila ya wachache, watu wenye ulemavu na masikini.

Bwana Laso amesema uhamiaji lazima utambulike kama ni moja ya mikakati muhimu katika suala la mazingira, hivyo watu hawa lazima wawe na fursa ya kuweza kuhama na sera za uhamiaji lazima zitilie maanani suala la mazingira.

(SAUTI YA PILAR ALVAREZ-LASO)

Taarifa hiyo pia imependekeza kuzingatia haki za za binadamu za watu walioathirika na mabadiliko ya hali ya hewa na kufuatia uhusiano uliopo baina ya uhamiaji na mabadiliko ya hali ya hewa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter