Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaeleza umuhimu wa lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV

WFP yaeleza umuhimu wa lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP katika kuadhimisha siku ya ukimwi duniani limetoa msisitizo kuhusu umuhimu wa kuwapa chakula na msaada wa lishe watu wanaoishi na virusi vya HVI pamoja na familia zao.

Kwa mujibu wa mkuu wa lishe na sera za HIV na ukimwi wa WFP Martin Bloem shirika hilo limekuwa likishirikiana na jamii na vituo vya aya kote duniani kuhakikisha watu walioathirika na virusi vya HIV na ukimwi wanapata msaada unaohitajika wa lishe ili kuimarisha afya zao. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)