Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi dhidi ya ubalozi wa uingereza Tehran

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi dhidi ya ubalozi wa uingereza Tehran

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu vikali mashambulizi yaliyofanywa kwenye ubalozi wa uingereza nchini Iran, mashambulizi yaliyosababisha uharibifu kwenye makao ya ubalozi huo.

Vyombo vya habari vinasema kuwa waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwenye mji mkuu Tehran walivunja na kuingia kwenye makao ya ubalozi wa uingereza wakipinga vikwazo vilivyowekwa na uingereza ambapo walichoma bendera ya nchi hiyo na kupasua madirisha ya majengo ya ubalozi. Wanachama wa Baraza la Usalama la UM wametoa wito kwa Iran kulinda mali na wafanyikazi wa balozi.