Teknolojia ya setilaiti inasaidia katika misitu:FAO

30 Novemba 2011

Utafiti mpya unaofanyika kwa njia ya setilaiti na kutolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO unaonyesha picha kamili ya mabadiliko katika misitu duniani.

Picha hiyo inaonyesha kwamba matumizi ya ardhi ya misitu imepungua kati ya mwaka 1990 na 2005. Kwa mjibu wa utafiti huo wa satellite maeneo ya misitu kwa mwaka 2005 ilikuwa ni ekari bilioni 3.69 sawa na asilimia 30 ya ardhi ya dunia.

Ripoti inasema kiwango cha ukataji miti kwa ajili ya ardhi ya kilimo kwa wastani ni ekari milioni 14.5 kwa mwaka kati ya mwaka 1990 hadi 2005 ambayo inalingana na makadirio yaliyopita. Adam Gerrand afisa wa misitu wa FAO.

(SAUTI YA ADAM GERRAND)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter