Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji zaidi katika vita vya Ukimwi unahitajika licha ya mafanikio:WHO

Uwekezaji zaidi katika vita vya Ukimwi unahitajika licha ya mafanikio:WHO

 

Hatua zilizopigwa kimataifa katika kuzuia na matibabu ya HIV zinasisitiza faida ya kuwekeza katika vita dhidi ya maradhi hayo kwa muda mrefu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika la afya duniani WHO kwa ushirikiano na shirika la kuhudumia watoto UNICEF na lile la kupambana na ukimwi UNAIDS. Ripoti hiyo iitwayo “Taarifa ya mapambano ya HIV na ukimwi kimataifa” inaonyesha kwamba ongezeko la upatikanaji wa huduma za HIV imepunguza maambukizi mapya kwa asilimia 15 katika muongo uliopita na kupunguza vifo vya ukimwi kwa asilimia 22 katika miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa WHO kitengo cha ukimwi Gottfried Hirnschall imeichukua dunia miaka kumi kufikia kiwango hicho na kwambba maendeleo katika sayansi na ubunifu mwaka jana unaongeza matumaini ya baadaye ya vita dhidi ya ukimwi.

(SAUTI YA GOTTFRIED HIRNSCHALL)