Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la makombora ndani ya Israel kutoka Lebanon

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la makombora ndani ya Israel kutoka Lebanon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani kurushwa kwa makombora mawili ndani ya Israel kutoka kusini mwa Lebanon Jumanne.

Vikosi vya ulinzi vya Israel vimeripotiwa kurejesha moto kuelekea mahali ambako makombora yametoka.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa Israel na Lebanon kujizuia kuendeleza vitendo hivi na kuheshimu mkataba wao wa kumaliza vita. Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduardo Del Buey anasema mpango wa Umoja wa Mataifa Lebanon UNIFIL umeanza uchunguzi wa tukio hilo.

(SAUTI YA EDUARDO DEL BUEY)