Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo ya fedha sio sababu ya kutopambana na umasikini

Matatizo ya fedha sio sababu ya kutopambana na umasikini

Matatizo ya kiuchumi yanayoikabili dunia hivi sasa yasiwe sababu ya mataifa tajiri kutotimiza wajibu wao wa ahadi walizotoa kwa nchi zinazoendelea. Huo ni ujumbe aliorejea kuutoa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipowasili Busan, Korea ya Kusini Jumanne.

Ban anahudhuria mkutano wa serikali na sekata binafsi unaojadili umuhimu wa misaada. Amesema majadiliano hayo Busan ni lazima yatoe ujumbe wa pamoja kwamba dunia bado imejidhatiti kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya kutokomeza umasikini uliokithiri ifikapo mwaka 2015. Martin Nesirky ni msemaji wa Katibu Mkuu.

(SAUTI YA MARTIN NESIRKY)