Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya kilimo inahitaji kupunguza kutegemea nishati inayotoka kwa mimea:FAO

Sekta ya kilimo inahitaji kupunguza kutegemea nishati inayotoka kwa mimea:FAO

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa sekta ya kilimo duniani inahitaji kupunguza kutegemea kwake kwa nishati inayotokana na mimea ili iweze kufanikiwa kulisha idadi ya watu inayoendelea kuongezeka duniani.

FAO inasema kuwa hali ya kutegemea nishati inayotokana na mimea huenda ikaathiri uwezo wa sekta ya kilimo katika kuafikia malengo yake. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)