Changamoto mpya za kutoa huduma za kibinadamu zashuhudiwa Somalia

29 Novemba 2011

Oparesheni za kijeshi zinazoendelea nchini Somalia pamoja na mvua kubwa inayonyesha vimetajwa kuzuia kuhama kwa watu kwenye eneo la Gedo lililo karibu na mpaka na Kenya. Mvua inayonyesha imeifanya barabara kutopitika huku wengi wakihofia kujikuta kwenye mapigano wanapohama.

Hata hivyo kuna ripoti za zaidi ya watu 500 walio safarini wakiwemo watoto wanaosafiri kutoka Qooqaani, Tabta na Afmadow wakielekea mji ulio kwenye mpaka wa Dobley. Tangu mwezi Oktoba watu 8300 wamelazimika kuhama mji wa Mogadishu kutokana na mizozo huku 500 wakihama kutokana na ukame. Andrej Mahecic msemaji wa UNHCR anaripoti.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)

Vile vile bwana Mahecic amesema kuwa katika Kambi ya Dollo Ado nchini Ethiopia kumeshuhudiwa viwango vya juu vya utapiamlo miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter