Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea zisaidiwe kwenye teknolojia ya nishati UNCTAD

Nchi zinazoendelea zisaidiwe kwenye teknolojia ya nishati UNCTAD

Majadiliano ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na uchumi unaoathiri mazingira yametajwa kuwa yenye manufaa makubwa kwa nchi zinazoendelea.

Ripoti ya shirika la bishara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD mwaka 2011 inapendekeza kusaidiwa kwa mataifa yanayoendelea katika masuala ya teknolojia hasa kwenye nishati inayorudiwa. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema kuwa jitihada za kimataifa zinahitajika kufanywa kuhakikisha kupatikana kwa kawi akiongeza kuwa Umoja wa Mataifa umeutangaza mwaka 2012 kama mwaka wa kimataifa wa nishati kwa wote. George Njogopa ana taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)