Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazipongeza Somali, Afrika ya Kati juu ya mpango wake wa kuachana na utumiaji watoto kama askari

UM wazipongeza Somali, Afrika ya Kati juu ya mpango wake wa kuachana na utumiaji watoto kama askari

Umoja wa Mataifa umepongeza dhamira iliyowekwa na nchi za Jamhuri ya Kati na Somalia ambazo zimekubali kutoendelea kuwatumia watoto katika sehemu za vikosi vyake. Nchi hizo kwa pamoja zimeafikiana kusitisha kabisa utumiaji watoto kuwa sehemu ya askari wake na kuhaidi kuleta mafungamano mapya hasa wakati huu kunajitokeza miito ya umalizwaji wa siasa za uhasama.

Hata hivyo pamoja na kupongeza hatua hiyo, mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa Radhika Coomaraswamy amesema kuwa bado nchi zote zinakabiliwa na hali ya mkwamo na zinapaswa kuweka nira ya kweli ili kufikia shabaya hiyo. Somalia ni miongoni mwa nchi mbili duniani ambazo haziridhi mkataba wa Umoja wa Mataifa unaoangazia haki za watoto.