Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi unaojali mazingira ni mkombozi wa kweli

Uchumi unaojali mazingira ni mkombozi wa kweli

Uwekaji wa zingatia juu ya uchumi unaojali mazingira ni fursa tosha inayotoa uhalisia wa mambo lakini hata hivyo viongozi wa dunia wanapaswa kuupa msukumo mpango huo ili upate mafanikio.

Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na maendeleo ya viwanda UNIDO Kandeh K. Yumkella ambaye ameongeza kusema kuwa uchumi unaojali mazingira una agenda muhimu kwa maendeleo ya dunia.

Akizungumza mjini Vienna kwenye kongamano, Yumkella amesema kuwa Umoja wa Mataifa unaendelea kusalia nafasi ya mbele kuhimiza ulimwengu juu ya kuweka zingatio kwenye uchumi unaojali mazingira.

Ametaja kusudia la mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa unaojulikana kama (Rio+20) ambao utafanyika mwaka kesho kuwa ndiyo jukwaa muhimu la kupima mwelekeo wa dunia kuhusu mazingira na maendeleo.