Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazungumzia dhuluma za kingono nchini Ivory Coast

UM wazungumzia dhuluma za kingono nchini Ivory Coast

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaoongoza jitihada za kupambana na dhuluma za kingono kwenye mizozo umeitaka serikali na viongozi wote wa kisiasa nchini Ivory Coast kulipinga suala hilo na kuhakikisha halitumiki kuwadhulumu watu kabla ya uchaguzi wa ubunge uanaotarajiwa kuandaliwa mwezi ujao.

Haya ni kwa mujibu wa mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya dhuluma za kingono kwenye mizozo Margot Wallatrom alipofanya ziara rasmi nchini Ivory, ambapo pia alikutana na mawaziri wa serikali , maafisa wa ngazi za juu kwenye idara ya polisi na waathirwa wa dhuluma za kingono. Amesisitiza kuwa mengi yanahitajika ili kuwasaidia wanaodhulumiwa kingono nchini Ivory Coast.