Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yajumuisha tamaduni 12 kwenye orodha yake

UNESCO yajumuisha tamaduni 12 kwenye orodha yake

Tamaduni 12 zikiwemo za kupanda mchele nchini Japan, Muziki wa Mariachi nchini Mexico pamoja na tamaduni za mbio za farasi nchini Ufaransa zimejumuishwa kwenye orodha inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ya tamuduni za kale.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ni kwamba kamati ya wanachama 24 inayokutana kwenye kisiwa cha Bali nchini Indonesia ilijuuisha tamaduni hizo kwenye vikao viwili hii leo.

Pia tamaduni mbili kutoka nchini Croatia zilijumuishwa kwenye orodha hiyo zikiwemo za kuimba na kucheza kutoka kwa jamii ya Bacarac mashariki mwa nchi.