Ban asikitika kufuatia kuendelea kwa ghasia Misri:

28 Novemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka serikali ya mpito ya Misri kuzingatia maslahi ya demokrasia na uheshimuji wa haki za binadamu katika wakati ambapo kukiripotiwa kuzuka kwa machafuko yaliyosababisha mauwaji ya watu kadhaa.

 Ban amesema amesikitishwa na kuzorota kwa hali ya kisiasa na amesisitiza kuwa serikali ya mpitio inawajibika kulinda haki za binadamu.

 Kiasi cha watu 30 wamepoteza maisha wakati vikosi vya serikali vilipojaribu kuyadhibiti maandamano ya wananchi wanaandamana wakitaka kuwepo kwa utawala wa kiraia. Duru la kwanza la uchaguzi wa wabunge inafanyika leo jumatatu.

Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na mkuu wa baraza la kijeshi Mohammed Hussein Tantawi, Ban amesema kuwa utawala huo wa mpito unawajibika kulinda na kuzijali haki za binadamu .

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter