Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka miwili ijayo muhimu kwa haki za binadamu:Pillay

Miaka miwili ijayo muhimu kwa haki za binadamu:Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema Jumatatu kwamba miaka miwili ijayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya taasisi za haki za binadamu za kitaifa na kanda ya Asia, hususani katika hali ya mabadiliko inayoendelea nchini Myanmar taifa litakalokuwa mwenyekiti wa ASEAN mwaka 2014.

Pillay amekuwa katika ziara ya siku tatu kwenye kisiwa cha Bali Indonesia ambako mkutano wa ASEAN unafanyika ukihusisha tume za kitaifa za haki za binadamu, taasisi za kitaifa za haki za binadamu kutoka mataifa manne ya ASEAN na jumuiya za kijamii.

Akiwa Bali Pillay amezungumza kwa njia ya simu na mwanaharakati Daw Aung San Suu Kyi na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo uwenyekiti wa ASEAN wa Myanmar mwaka 2014 na pia umuhimu wa maendeleo ya haki za binadamu katika taifa hilo na kanda nzima.