Kenya yatoa hati ya kukamatwa Rais Al-Bashir wa Sudan

28 Novemba 2011

Mahakama ya Kenya imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar Al-Bashir anayekabiliwa na madai ya uhalifu wa kivita kwenye jimbo la Darfur. Uamuzi huo umetolewa baada ya serikali ya Kenya kumruhusu Rais Bashir kuzuru nchini humo mwezo Agosti. Ikipingana na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC ambayo imekuwa ikisisitiza kukamatwa kwa bwana Bashir.

Duru za habari kutoka Kenya zinasema jaji wa mahakama  Nicolas Ombija amesema Bashir anapaswa kukamatwa iwapo atakanyaga tena Kenya. Kenya ni moja ya nchi ziliazoridhia mkataba wa kuundwa kwa ICC mwaka 2002. Bashir ni Rais wa kwanza kushitakiwa na mahakama ya ICC inayomshutumu kwa mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita uliotekelezwa kwenye jimbo la Darfur.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud