Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inahitaji dola milioni 40 kuendesha operesheni hadi mwisho wa mwaka

UNICEF inahitaji dola milioni 40 kuendesha operesheni hadi mwisho wa mwaka

Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Rima Salah amehitimisha ziara ya wiki moja katika mataifa ya Ghuba iliyokuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano wa kukabiliana na matatizo ya kibinadamu.

Katika ziara yake Salah amekuwa na mazungumzo na wawakilishi wa serikali, mashirika ya kimataifa na wadau wengine. Salah alizuru kwanza Jeddah Saudia akiwa na mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Kibinadamu Bi Valerie Amos ambaye ametia saini mkataba wa maelewano na jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiislamu OIC. Amesema lengo ni kushirikisha kikamilifu jumuiya hiyo yenye wanachama zaidi ya mataifa 50 na kwamba baadhi ya matafa ya jumuiya hiyo kama Saudia, Qatar na Falme za Kiarabu yanashirikiana na UNICEF na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali kusaidia janga la kibinadamu linaloendelea Somalia.

Ameongeza kuwa ili UNICEF kuweza kukabiliana na operesheni zote za dharura hadi mwisho wa mwaka huu wa 2011 dola milioni 40 zinahitajika.

(SAUTI YA RIMA SALAH)