Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito wa mshikamano kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa watolewa: UM

Wito wa mshikamano kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa watolewa: UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binadamu na mshikamano wa kimataifa Virginia Dandan amewataka wachafuzi wa hali ya hewa wapya na wa muda mrefu kuwa vinara katika majadiliano ya mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoanza Jumatatu Durban Afrika ya Kusini.

Bi Dandan amewataka pia kutoa shinikizo la kimataifa katika kukinga zaidi kuliko kuchukua hatua baada ya athari zilizosababishwa na majanga ya asili na shughuli za binadamu. Amesema mshikamano wa kimataifa ni muhimu sana kupambana moja kwa moja na changamoto za kimazingira za kimataifa. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)