Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia za uchaguzi zaendelea DRC

Ghasia za uchaguzi zaendelea DRC

Kunaripotiwa ghasia zinazohusiana na uchaguzi wa urais na ubunge unaotarajiwa kuandaliwa tarehe 28 mwezi Novemba kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ukiwa ndio uchaguzi wa pili kuandaliwa nchini DRC tangu mwaka 2006.

Zaidi ya wapiga kura milioni 32 wanatajariwa kupiga kura ya kumchagua rais huku zaidi ya wagombea 18,000 wakitarajiwa kuwania viti 500 za ubunge. Madnodje Mounoubai ambaye ni msemaji wa MONUSCO anafafanua baadhi ya changamoto zinazokumba uchaguzi huu.

(SAUTI YA MADNODJE MOUNOUBAI)