Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yatoa ripoti kuhusu kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa

UNEP yatoa ripoti kuhusu kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limetoa ripoti mpya inayoelezea hatua ambazo ikiwa zitatekelezwa kote duniani zitasaidia katika kuokoa maisha ya watu milioni 2.5 na kuzuia kupotea kwa tani 32 za chakula kila mwaka.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa hatua hizo zitasaidia kupunguza kupanda kwe joto duniani hata hadi kati kati ya karne hii. Kati ya hatua zilizotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na kupunguzwa kwa gesi chafu. Ripoti hiyo iliyofadhiliwa na serikali ya Sweden inakadiria kuwa kupunguzwa kwa nusu gesi za Carbon na Methane kunaweza kuafikiwa kwa njia nafuu na rahisi.