Watu zaidi bado wanahitaji misaada nchini Pakistan

25 Novemba 2011

Zaidi ya watu milioni 5 kwa sasa wanahitaji huduma za kinidamu kwenye mikoa ya Sindh na Bolichistan nchini Pakistan huku asilimia 25 wakiwa ni wanawake na asilimia 50 wakiwa ni watoto. Huku nyumba 797,000 zikiwa zimeharibiwa kwa sasa takriban watu milioni 1.2 wanaorejea makwao wanahitaji nyumba zao kurekebishwa au kujengwa upya.

Tangu mwezi Oktoba mafuriko yamepungua katika sehemu zilizoathirika. Watu wengine 660,000 kwenye mkoa wa Sindh na zaidi ya wengine 83,800 kwenye mkoa wa Balochistan hawana makao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa misaada ya makao 35,000 na misaada mingine ikiwemo mablanketi, matandiko ya kulalia na vyombo vya jikoni. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa Shirika hilo

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter