Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU na washirika kupelekeza mapendekezo kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

ITU na washirika kupelekeza mapendekezo kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

Chama cha kimataifa cha mawasiliano ITU kwa ushirikiano na washikadau kwenye sekta ya kiviwanda watafanya jaribio la kuwashawishi wajumbe kwenye mkutano kuhusu mabadilliko ya hali ya hewa ambao utaandaliwa mjini Durban wiki ijayo kama moja ya njia ya kuimarisha njia za teknolojia ya mawasiliano.

Teknolojia za kisasa zina uwezo wa kuboresha masuala ya kijamii, kiviwanda na kibiasahara tatizo ni kuwa teknolojia hii haitambuliwi na mashirika ya kimazingira.

ITU na washirika wake watautumia mkutano huo kuonyesha kuwa teknolojia ya mawasiliano ni kiungo muhimu katika kutatua matatizo kwenye karne ya 21.

Alice Kariuki na taarifa kamili

SAUTI YA ALICE KARIUKI