Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR kuwahamisha wakimbizi 20,000 nchini Sudan Kusini

UNHCR kuwahamisha wakimbizi 20,000 nchini Sudan Kusini

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR lina mipango ya kuwahamisha wakimbizi 20,000 kwenda maeneo salama nchini Sudan Kusini kutokana na kuchacha kwa ghasia kwenye mpaka kati ya Sudan Kusini na Sudan.

Wakimbizi waliokimbia mapigano kutoka majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini wamepiga kambi kwenye mji wa Yida ambao ulishambuliwa na ndege za Sudan mapema mwezi huu.

UNHCR imewaandalia wakimbizi hao eneo kwenye jimbo la Unity ambapo inatarajia kuwahamisha kwa hiari wakimbizi hao. Naibu mkurugenzi wa UNHCR kwenye pembe ya Afrika Raouf Mazou anasema kuwa huenda wakimbizi zaidi wakahamia Sudan Kusini na Ethiopia ifikapo mwishoni mwaka huu.

(SAUTI YA RAOUF MAZOU)