Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu huambukizwa magonjwa wakiwa hospitalini: WHO

Watu huambukizwa magonjwa wakiwa hospitalini: WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa mmoja kati ya watu 10 kwenye nchi zinazoendelea huwa anaambukizwa ugonjwa akiwa hospitalini kutokana na huduma duni za kiafya. IIi kukabiliana na tatizo hili WHO imezindua ushirikiano kati ya hospitali za Ulaya na Afrika ili kuimarisha usafi na huduma zingine .

Hospitali za uswisi zimekuwa zikishirikiana na hospitali nchini Cameroon , Mali, Senegal huku hospitali za uingereza zikishirikiana na zile za Ethiopia, Malawi na Uganda kiafya.

Daktari Tonny Tumwesigye mkurugenzi wa Hospitali ya Kisizi mjini Kabale Uganda anasema kuwa suala la madaktari la kutonawa mikono limesahaulika hali ambayo imepunguza maambukizi ya magonjwa.