Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waweka msukumo kuokoa maisha ya ndege wanaopoteza maisha kutokana na nyaya za umeme

UM waweka msukumo kuokoa maisha ya ndege wanaopoteza maisha kutokana na nyaya za umeme

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Mazingira UNEP limesema kuwa maelfu kadhaa ya ndege hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kuangukia kwenye mifumo ya umeme na wakati huo huo ndege wengine zaidi ya milioni 5 hugongamana na mifumo ya kusafirishia umeme katika zone ya Afrika Ulaya.

Shirika hilo limeonya juu ya hatari ya mitambo ya kusambaza umeme kuendelea kupoteza maisha ya ndege wengi duniani.

Katika eneo la Afrika na Ulaya ripoti zinaonyesha kuwepo kwa vifo vingi vya ndege vinavyosababishwa na mitambo ya kusambazia umeme ama kugonga kwenze mringoti yake.

Ili kujaribu kusaka njia muaafaka ya kunusuru hali hiyo, watalaamu kadhaa wanakutana huko Norway ambako wanajadilia msauala kadhaa juu ya kupunguza kiwango cha vifo vya ndege.