UNHCR yaikata Uingereza kuwajali watu wasio na makwao

25 Novemba 2011

 

Ripoti moja iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR imesema kuwa watu wanaoishi nchini Uingereza ambao siyo raia wa nchi hiyo wanakabiliwa na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu.

 Ripoti hiyo imeitaka Uingereza kuchukua hatua za haraka kurekebisha hali hiyo na kuongeza kuwa mamlaka za dola zinapaswa kuweka mazingira huru na salama kwa shabaya ya kulinda ustawi wa wahamiaji hao.

 Katika ripoti yake hiyo UNHCR imesema kuwa utafiti wake uliofanya kwenze maeneo mbalimbali nchini humo unaonyesha hali ya dhiki na taabu wanaokutana nao watu hao.

Imesema wakati mwingine watu hao wasiokuwa na makwao wanaishi kwenye mazingira ya hatari na hata kulazimika kuishi mitaani na sehemu nyingine zisizo rasmi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud