Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN, MTV waanzisha kampeni kukabili vitendo vya utumikishaji vijana

UN, MTV waanzisha kampeni kukabili vitendo vya utumikishaji vijana

Taasisi kadhaa za kimataifa ikiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF zimeanzisha kampeni maalumu yenye shabaya ya kutuma ujumbe kwa dunia kuhusiana na madhira yatokanayo na biashara ya usafirishaji watu.

Kampeni hiyo ambayo pia inahusisha vituo kadhaa vya television ikiwemo kituo cha muziki cha MTV, imelenga kuleta uelewa zaidi juu ya madhara ya utumikishaji vijana kwa jamii ya Hispania.

Kampeni hiyo inayojulikana kama ‘MTV EXIT’, imekusanya masuala mbalimbali ikiwemo nyimbo pamoja na filamu ambazo zinaangazia kwa kina athari za utumikishaji vijana.

Kwa mujibu wa takwimu za UNICEF zaidi ya vijana 550,000 wametumbukia kwenye athari za utumikwishaji katika eneo la Latin Amerika na katika visiwa vya Carebean. Wengi wao wametumbukizwa kwenye vitendo vya ngono isiyo salama na ubwiaji madawa ya kulevya.