Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azipongeza Cameroon, Nigeria kufuatia kumalizika mgogoro wa mpaka

Ban azipongeza Cameroon, Nigeria kufuatia kumalizika mgogoro wa mpaka

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifaa Ban Ki-moon amezipongeza nchi za Cameroon na Nigeria kwa kutekeleza kikamilifu hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ICJ juu ya mzozo wa mpaka baina ya pande zote mbili. Pande hizo zimeridhia kutekeleza maamuzi ya mahakama hiyo ya kimataifa ambayo ilizitaka kugawana maeneo ya mipaka kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na mahakama hiyo.

Ban amezipongeza nchi hizo akisema kuwa zimefaulu kutekeleza maazimio ya makahaka ya kimataifa bila mikwaruzani yoyote. Hatua hiyo sasa inazika uhasama wa miaka mingi uliosababisha machafuko ya mipakani baina ya wananchi wa pande zote mbili.