Mtanzania ashinda shindano la UNiTE la vita dhidi ya ukatili kwa wanawake

24 Novemba 2011

Mwanafunzi wa chuo kikuu kutoka nchini Tanzania Mwasapi Kohongosi ameshinda shindano la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la UNiTE la kampeni ya kumaliza ukatili dhidi ya wanawake kwa kubuni T-shirt.

Mwasapi mwenye umri wa miaka 23 amesema anafuraha kubwa sana na ni suala ambalo hakulitegemea maishani ingawa amekwa akibuni michoro kwa muda mrefu.

Mwasapi amekabidhiwa tuzo yake rasmi na Katibu Mkuu Ban Ki-moon Jumatano November 23 kwenye makao maku ya Umoja wa Mataifa hapa New York katika hafla maalumu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga katili dhidi ya wanawake.

Akizungumza na mwandishi wa Umoja wa Mataifa Stella Vuzo kabla ya kuondoka Dar es saslaam kuja New York kupokea tuzo hiyo Mwasapi hakuusita kdhuhirisha furaha yake.

(MAHOJIANO NA MWASAPI 1)

Naam na ujumbe wake ameuwasilisha vilivyo kwa Bank Ki-moon. Mwasapi ambaye ni mwanafunzi wa compter science kutoka chuo kikuu cha Dar es slaam ni miongoni mwa washindi wengine watano kutoka mabara yote duniani ikiwemo Uulaya, Asia, Amerika ya Kusini, Marekani, Australia na ushindi wake unaliwakilisha bara la Afrika. Endelea kusikiliza mahojiano yake na Stella Vuzo.

(MAHOJIANO NA MWASAPI 2)