Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna haja ya kumaliza hali ya sasa na kuanza tena mazungumzo mashariki ya kati:Ban

Kuna haja ya kumaliza hali ya sasa na kuanza tena mazungumzo mashariki ya kati:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza kwa njia ya simu Jumatano na waziri mkuu wa Israel, amesisitiza haja ya kumaliza hali ya sasa ili kuweza kuweka mazingira mazuri ya kufufua mazungumzo ya moja kwa moja ya amani baina ya Israel na Palestina.

Ban amemtaka waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuanza mara moja kuhamisha kodi na mapato ya Palestina kwa kuzingatia wajibu wa kisheria za Israel. Pia ameelezea hofu yake kufuatia tangazo la Israel la kupanua zaidi makazi ya Walowezi ikiwemo Jerusalem Mashariki hali ambayo inatia dosari juhudi za mchakato wa amani na pia inakiuka sheria za kimataifa. Ban amekaribisha hatua ya Israel ya kuidhinisha miradi mipya ya Umoja wa Mataifa ya ujenzi Gaza inayogharimu dola milioni 5.5 huku akitioa wito wa hatua za kutekeleza azimio la Baraza la Usalama namba 1860.