Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lengo la kufikia nyuzi joto chini ya 2 hapo 2020 inawezekana:UNEP

Lengo la kufikia nyuzi joto chini ya 2 hapo 2020 inawezekana:UNEP

Kupunguza gesi chafu ifikapo mwaka 2020 na kufikia kiwango kitaiweka dunia katika karne ya 21 kwenye joto la chini ya nyuzi 2 , kiteknolojia na kiuchumi ni jambo linalowezekana umesema utafiti mpya wa shirika la moja wa Mataifa la mazingira UNEP uliochapishwa Jumatano.

UNEP inasema matumizi ya kuimarika kwa nishati mbadala, kupunguza matumizi ya mafuta na matumizi bora kunaweza kuchangia pakubwa kupunguza gesi chafu lakini pia hatua zingine zinahitajika ikiwemo kuboresha sekta za usafiri, kutumia magari yanayojali mazingira hasa katika sekta ya kilimo na pia kudhibiti taka.

Ripoti hiyo ya UNEP iliyoitwa “kuziba pengo la utoaji gesi chafu” imetolewa siku chache tuu kabla ya mjadala wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa utakaoanza nchini Afrika ya Kusini Jumapili na ni miezi saba tu kabla ya mkutano wa Rio+20 nchini Brazil. Ripoti hiyo inaainisha bayana kwamba dunia tayari ina suluhu ya kukwepa athari zaidi za mabadiliko ya hali ya hewa.