Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wanaweza kusaidia kumaliza ukatili dhidi ya wanawake

Vijana wanaweza kusaidia kumaliza ukatili dhidi ya wanawake

Vijana duniani kote wamechagizwa kuwa msitari wa mbele katika kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Wito huo umetolewa Jumatano katika maadhimisho ya 15 ya mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake. Siku hii pia Umoja wa Mataifa unasherehekea siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake.

Mfuko wa Umoja wa Mataifa umejikita katika kusaidia juhudi za kimataifa na kimataifa katika kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na umeshatoa zaidi ya dola milioni 78 kwa mamia ya miradi katika kipindi cha miaka 15. Viongozi vijana kutoka kote duniani wamekutana mjini New York ili kujadili suala la hili na mwenyeji wa mkutano huo ni UN Women chombo kilichoanzishwa Julai mwaka jana ili kuchapuza lengo la usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.