Pillay alaani jeshi na vikosi vya usalama kwa kuuwa waandamanaji nchini Misri

23 Novemba 2011

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay Jumatano amelaani jukumu la jeshi na vikosi vya usalama nchini Misri kwa kujaribu kukandamiza waandamanaji katika siku tano zilizopita na hususani taarifa za kuuawa waandamanaji zaidi ya 30 na wengine wengi kujeruhiwa. Waandamanaji hao wanadai kurejea kwa utawala wa kiraia nchini humo.

Pillay ameutaka uongozi wa Misri kusitisha matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji hao waliokusanyika Tahir Square na kwingineko nchini humo. Pillay ameyataka majeshi yaache kutumia mabomu ya machozi, risasi za mpira na risasi za kawaida. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud