Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili ni moja ya vikwazo vikubwa kwa wanawake kupata usawa:Ban

Ukatili ni moja ya vikwazo vikubwa kwa wanawake kupata usawa:Ban

Wanawake na wasichana wote wana haki ya kuishi kwa uhuru bila ukatili, na haki hii imeainishwa kwenye misingi ya kimataifa ya haki za binadamu na sheria za kimataifa amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Ban ameyasema hayo Jumatano kwenye hafla maalum ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake. Ban amesema suala hilo ni kitovu cha mpango maalumu aliouanzishwa wa UNITE ambao ni kampeni ya kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Ameongeza kuwa pamoja na vita vya kumaliza ukatili huo changamoto ni kuhakikisha ujumbe wa uvumilivu sufuri dhidi ya ukatili unasikika kila kona ya dunia, na kuhakikisha hilo ni lazima kuzihusisha jamii zote na hususani vijana, wavulana.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)