Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaohusika kwenye uharamia wachukuliwe hatua:UM

Wanaohusika kwenye uharamia wachukuliwe hatua:UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vitendo vya utekaji nyara vinavyoendelea kwenye pwani ya Somalia likisema kuwa vitendo vya uharamia vinaendelea kutishia usalama na amani katika eneo hilo.

Kwenye azimio lililopitishiwa bila kupingwa na baraza hilo linataka kufanywa uchunguzi na kuwahukumu sio tu washukiwa wanaokamatwa baharini bali pia wale wanaochangia kuwepo kwa uharamia. Baraza hilo linatoa wito kwa mataifa yaliyo na uwezo wa kupambana na uharamia kufanya hivyo kuambatana na sheria za kimataifa.