Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanzisha majadiliano ya kimataifa juu ya maendeleo endelevu inayojali mazingira

UM waanzisha majadiliano ya kimataifa juu ya maendeleo endelevu inayojali mazingira

Kuna haja ya kukuza maendeleo endelevu na miji imara, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliwaambia wajumbe katika kampeni ya kuhamasisha mkutano mkuu wa mabadiliko ya hali ya hewa nchini Brazil.

Rio +20, Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo Endelevu, utafanyika mjini Rio de Janeiro mwezi Juni mwaka ujao.

Dunia inakabiliwa na mlolongo wa changamoto, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, kuongezeka kwa uzalishaji wa gesi ya cabon na bahari chafu, alisema Bw Ban.

Aliongeza Rio 20+ ni fursa ya kipekee ya kujadili ufumbuzi wa matatizo haya.

Rio+ 20 itahamasisha watu kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya kimataifa kuhusu matarajio yao ya siku za usoni yatakayoongeza ustawi na kuimarisha maisha ya watu bila kuharibu mazingira.