Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba wa misaada kwa waathiriwa wa mafuriko washuhudiwa Pakistan

Uhaba wa misaada kwa waathiriwa wa mafuriko washuhudiwa Pakistan

Huenda asilimia kubwa ya watu milioni 5 walioathiriwa na mafuriko mwaka huu nchini Pakistan wakakosa usaidizi. Hii ni kulingana na shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linalosema kuwa ni asilimia 35 ya ombi la dola milioni 357 lililotolewa na wafadhili hadi sasa.

OCHA inasema kuwa hali hii huenda ikachangia uhaba wa chakula, makao na maji pamoja na hali mbaya ya usafi na kuyaweka hatarini maisha ya maelfu ya watu. Kulingana na serikali ya Pakisatan ni kuwa idadi ya waliokufa kutokana na mafuriko imefikia watu 466 huku watu 756 wakijeruhiwa. Stacey Winston kutoka OCHA alizungumza na radio ya UM.

(SAUTI YA