Ghasia zapamba moto Misri kati ya polisi na waandamanaji

22 Novemba 2011

Kunaripotiwa kuongezeka kwa makabiliano kati ya waandamanaji na polisi kwenye eneo la Tahir Square kwenye mji mkuu wa Misri Cairo kwa siku ya nne mfululizo. Raia nchini Misri wamekuwa wakikasirishwa na kujikokota kwa jeshi katika kubadili utawala wa nchi hiyo kuwa wa kiraia huku watu wengi wakiingia mitaani baada ya kushuhudia kupitia kwa runinga watu wakiuawa na vikosi vya wanajeshi.

Watu 33 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa tangu siku ya Jumamosi. Ghasia hizi zinajiri siku chache kabla ya uchaguzi wa ubunge ambao ndio uchanguzi wa kwanza utakaoandaliwa tangu kupinduliwa madarakani kwa rais Hosni Mubarak.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud