Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Yemen akubali kusalimisha madaraka kwa naibu wake

Rais wa Yemen akubali kusalimisha madaraka kwa naibu wake

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jamal Benowar amesema kuwa rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh amekubali kutia sahihi makubaliano ya mabadiliko ambapo atasalimisha madaraka kwa naibu wake. Makubaliano hayo yanamaliza msukosuko wa kisiasa wa miezi kadhaa na machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.

Benomar anasema kuwa makamu wa rais wa Yemen atakuwa na madaraka yote makuu wakati wa kipindi cha mabadiliko kuhakikisha kutekelezwa kwa makubaliano hayo. Jamal Benomar aelezea.

(SAUTI YA JAMAL BENOMAR)

Makubaliono hayo yatamaliza uongozi wa miaka 30 wa rais Ali Abdullah Saleh.