Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahama ya ICC ndiyo itaamua itakaposikilizwa kesi ya Qadhafi:Ocampo

Mahama ya ICC ndiyo itaamua itakaposikilizwa kesi ya Qadhafi:Ocampo

Mwendesha mashataka mkuu kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Luis Moreno Ocampo amesema kuwa itakuwa ni uamuzi wa mahakama hiyo kuamua ni wapi mwana wa aliyekuwa rais wa Libya Saif Islam Qadhafi atahukumiwa kutokana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Ocampo ameyasema haya alipowasili mjini Tripoli akiandamana na naibu wake Fatou Bensouda kwa mazungumzo na tawala za nchi hiyo. Haya yanajiri kufuatia habari za kukamatwa kwa al- Islam Qadhafi na mkuu wa ujasusi Abdullah Al Sanaousi ambaye pia anatafutwa na mahakama hiyo. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)