Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Sierra Leone kuwasaidia waathirika wa ukatili wa kingono

UM waitaka Sierra Leone kuwasaidia waathirika wa ukatili wa kingono

Ofisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwenye maeneo yaliyokumbwa na machafuko ametaka kupatiwa msaada kwa manusura wa vitendo vya kingono nchini Siera Leona akiongeza kusema kuwa watu hawa wanapaswa kupewa msaada wa kisheria na haki ili waweze kurejea kwenze jamii zao.

Bi Margot Wallström,amesema kuwa makundi hayo ya watu yanapaswa kutiliwa zingatio la kipee kwa kupatiwa msaada wa hali na mali na ametaka mamlaka za kidola zinapaswa kusimamia haki na ukweli.

Akiwa kwenze ziara ya kuzitembelea nchi za afrika magharibu eneo ambalo limeshuhudia pakubw auvunjifu wa haki za kibinadamu,mwanadiplomasia huyo amegusia pia umuhimu wa kujenga mifumo madhabiti itayosaidia kuzuia kutojitokeza tena kwa vitendo kama hivyo. Akiwa nchini Siera Leone Margot anatazamia kufanya mazungumzo na maafisa mbalimbali.