Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM Somalia ataka kuzingatiwa kwa mpango wa ramani ya amani

Mjumbe wa UM Somalia ataka kuzingatiwa kwa mpango wa ramani ya amani

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ametaka kutekelezwa kwa mpango wa amani nchini humo ulioasisiwa Septemba wenye shabaha  ya kumaliza kipindi cha serikali za mpito.

Bwana Augustine Mahiga amesema kuwa kuna haja ya kutekelezwa kwa makubalino ya kupatikana kwa amani ya kudumu kwenzye eneo hilo na kusisitiza kuwa hatua hiyo inapaswa kutekelezwa sasa kabla ya kufikiwa ukomo wa serikali ya mpito hapo Agosti mwakani.

Mwanadiplomasia huyo amewatolea mwito viongozi wa Somalia akitaka watambue hatma ya nchi hiyo iko mikononi mwao na hivyo wanapaswa sasa kuongeza juhudi. Ustawi wa kisiasa nchini Somalia bado unaandamwa na mawimbi ya hapa na pale ikiwemo ukosefu wa hali ya amani na usalama.