Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima kuendelea mchakato wa amani Mashariki ya Kati:Serry

Lazima kuendelea mchakato wa amani Mashariki ya Kati:Serry

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Mashariki ya Kati leo amewatolea wito Israel na Palestina kujizuia kuchokozana na kuwasilisha mapendekozo ili kufufua mchakato wa amani na kuhusika katika majadiliano ya moja kwa moja.

Robert Serry ameliambia Baraza la Usalama akitoa taarifa ya maendeleo ya amani ya Mashariki ya Kati kwamba ni lazima kutafuta njia ya amani ya kidiplomasia kuendeleza machakato wa amani.

Ameongeza kuwa Israel na Palestina hivi karibuni zimekuwa zikifanya kazi kwa karibu na kundi la Quartet ambalo linajumuisha Umoja wa Mataifa, muungano wa Ulaya, Urusi na Marekani, hata hivyo amesema majadiliano ya amani kwa ana ambayo hayana masharti suala ambalo pande zote zinapaswa kuwakilisha hasa kuhusu masuala ya mipaka na usalama ndani ya siku 90 bado halijafanyika.

Serry amesema uchokozi unaendelea kuathiri majadiliano na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana kuwa ni vugumu sana. Zaidi ya hayo Israel inaendelea kupanua makazi ya Walowezi na kupinga ombi la Palestina la kutaka kuwa na uanachama kamili kwenye Umoja wa Mataifa.

Israel pia inashikilia dola milioni 1000 za mapato ya kodi ya Palestina kuafutia Palestina kupewa uanachama kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.